Mle garini akili haikuwa imetulia, fikra zake ziolikuwa mbali sana na pale barabarani. Bw. Nadama alikuwa akikumbuka majanga mengi ambayo alikuwa amepitia kwa miaka mitano aliyokuwa mshirika wa lile kanisa.
"Lakini bwana wee! Naogopa maneno ya watu," alikumbuka alivyomwambia rafikiye siku moja.
"You cannot prevent a bird from flying in the sky but you can stop it from nesting on your head," alikumbuka alivyojibiwa katikati ya kicheko.
Kicheko kile kilifanya akajiona mdogo zaidi ya mwenzake, alimwangalia tena kwa macho ya uoga. Walikuwa wanatoka matembezini mwendo wa saa mbili za usiku.
"Watasema mchana na usiku watalala, watakayokusimanga hayatajiandika usoni mwako," Bw. Vura aliendelea kumshawishi, "angalia nilivyoendelea kwa huu muda ambao nimekuwa katika kanisa hilo la mwanga.
Alikumbuka jinsi siku hiyo kutoka asubuhi walipoondoka nyumbani kwake, mazingumzo ya mwenzake yalikuwa juu ya mada hiyo moja mpaka wakati wa jioni walipokuwa wakirejea kutoka ziara zao.
"Lakini naogopa kumuasi Mungu!."
"Basi utaendelea kuishi katika umaskini wako."
"Hiyo ni kasumba."
"Si hivyo unavyofikiri, ulitima utakuandama siku zote. Utakuwa unalala na kuamkia umaskini kama mjalaana."
Baada ya maneno yale kila mmoja wao alikaa kimya, Bw. Nadama alikuwa anafikiri jinsi sahibu yake aliamua kumuasi Maulana kwa sababu ya kujipa mali kwa njia mbi. Walipofika nyumbani kwa rafikiye, walikaribishwa kwa manukato na harufu nzuri za vyakula ambavyo vilikuwa vikiandaliwa, alichukua kibaiskeli chake aina ya Hero kilichokuwa kimefungwa vibuyu vya kutembeza maziwa akaondoka.
Moyoni alijua rafikiye hakuwa amefanya uamuzi wa hekima alipoamua kufuata njia mbadala na ile ya uokovu.
"I better die poor than sin against God," alijiambia akipiga darubini dakika chache ambazo zilikuwa zimepita akakumbuka lile gari la kifahari ambalo alikuwa ametembelea.
Alipofika kwake alimpata mkewe Bi. Tabasuri akiwa ameketi nje na wana wao. Watoto wake was walipomuona walimkimbilia na kumlaki kwa furaha, mkubwa kwa jina la Labibu akachukua baiskeli. Walikaa wakipiga gumzo ya kifamilia kisha baada yake kula, watoto waliondoka.
Walipobaki na mkewe ndipo alipomsimulia yale ambayo yalikuwa yametokea.
"Heri wachawi tisini na tisa kuliko mnafiki mmoja," mkewe alimuonya, "huyo ni mnafiki, si rafiki. Mtu anayekujali hawezi kukupa ushauri wa kishenzi namna hiyo, ishindwe..."
Alijaribu kujiondolea zile fikra kwa kutikisa kichwa bila mafanikio, machozi yakamtoka bila kutarajia. Alijiona mpumbavu kwa sababu ya uamuzi ambao alikuwa amechukua
*****
"Stoop!!! Don't kill him," Labibu alitoa ukemi uliowafikia wazazi wake upande mwingine wa nyumba.
Bi. Tabasuri alijizoazoa kutoka kitandani baada ya kusikia sauti ya mwanawe. Alipofika katika chumba chake, aliwasha taa akamuona mwanambee wake amekaa katikati ya kitanda chake huku amevuta blanketi kwa nguvu. Alikuwa ameroa kwa jasho.
"Are you alright?!' mamake alimuuliza akiketi kando yake.
Labibu hata hakuweza kuitikia kwa kinywa, akaitikia kwa kutikisa kichwa, alikuwa anahisi uoga kama mtu ambaye alikuwa ameona kitu cha kuogofya.
"Nini tena usiku huu mwanangu?."
"I ...'ve had sa...me dr...e..a...m,"alimjibu mamake akitetemeka, "tu...li...kuwa msituni na mdogo wangu Guta tukitunda matunda walipotokea."
Mamake alimeikiliza kwa makini zaidi, ndoto iyo hiyo ya kutisha ilikuwa ikijirudia katika familia yake.
"Watu magwanda mekundu ka...ma damu wa...ka...tokea na ku...anza kutukimbiza," aliendelea kumsimulia mamake ndoto yake.
Kwa utaratibu babake alikuja na kusimama mlangoni akamwangalia mkewe, kisha akamgeukia mwanawe. Wote walikuwa wamevalia nyuso za hofu.
"Endelea," Bw. Nadama alimuamuru mwanawe.
"Wa...li...kuwa wamebeba mapanga, tulipokuwa tunakimbia, ulitokea lakini hata ulipotokea penyewe hatukuona, uli...ja...ri...bu kutuokoa lakini kwa bahati mbaya ulijikwa ukaanguka, kisha wale watu wakakufikia tayari ku...ku...angamiza. Ni...lipo...a...ngalia aliyeinua upanga, nilimuona Bw. Vura."
"Mimi...!" babake alimaka.
"Ndiyo."
"Ndipo nilipowaomba wasimuu..."
"Is it not same dream Guta had frequently before his death?!" Bi. Tabasuri alimkatiza mwanawe akimgeukia mumewe.
"Ndiyo, lakini mimi sina nguvu zozote kuikatiza," alimjibu mkewe akigeuka na kuanza kuondoka.
"Wachukulia vipi tukimyembelea Bw. Mhifadhi kesho na kumueleza haya!"
"Kesho nina shughuli muhimu za biash..."
"Shughuli muhimu za biashara," mkewe alimkatiza kwa kumrudishia maneno yake, "kwani hizo shughuli ni muhimu kuliko mwanao? Sio!."
"Si hivyo, vyote ni muhimu lakini ni heri nishughulikie haya Kwanza."
"Chaguo la kwanza ni biashara," mkewe alimwambia kwa uchungu, "he is obsessed with money that he even don't care about us."
Baada ya maneno yale chumba kilikuwa kimya, Labibu alikuwa amemkaribia kabisa mamake.
Pale mlangoni alipokuwa amesimama baada ya kusitisha muondoko wake alikuwa na mawazo chungu nzima, baada ya kuingizwa katika kanisa hilo na rafikiye Bw. Vura, hakuwa anataka kusikia neno lolote kutoka kwa makanisa mengine ndiposa alikuwa anasita kwa mwito wa mkewe kwenda kumuona mchungaji wake wa awali.
"Unaweza kumaliza ugeni wetu kwa mchungaji kisha ukaenda zako," mkewe alivunja kimya, "kwa sababu sitaraji kikao chenyewe kuzidi masaa mawili."
"Nishakusikia Bi. Mshauri, nitaenda ingawa shingo upande," Bw. Nadama alimjibu mkewe kisha akaondoka.
Bi. Tabasuri aliketi kando ya mwanawe akifikiri jinsi mumewe alikuwa amebadilika si kidogo. Aliona tofauti kubwa sana kati ya Nadama waliyefunga naye pingu za maisha na yule ambaye alikuwa akiishi naye kwa wakati huo.
Japo si kama Happ awali ambapo hata cha kutia kinywani walikuwa wakikosa, Nadama wa wakati huo hata alikuwa anapata pesa za kuistarehe familia yake, lakini mapenzi ya baba kwa wana yalikuwa yamepungua kwa asilimia kubwa.
Alikaa pale chumbani na mwanawe kwa dakika thelathini kisha akainuka na kumbusu pajini na kuanza kuondoka, kwa ghafla Labibu alimwangukia na kukamata guo lake.
"Usiniache mama!" Labibu alimlilia mamake, "naogopa."
"Unaogopa nini?!"
"Naogopa kuota tena, naogopa mama!."
"Ni sawa mwanagu," Bi. Tabasuri alimwambia, akarudi nakuketi kando yake.
"Do you think it will happen to him?!"
"Hapana mwanangu," mamake alimpa imani, "hiyo ni ndoto tu, isikutie hofu. Mungu tunayemtumikia atatulinda dhidi ya muovu shetani."
"Ni kweli Mungu hamuachi mja wake, ila siku hizi baba na ibada ni kama giza na mwanga. Kila siku ya Jumapili hutoa vijisababu ambavyo havina manufaa kukwepa kanisa."


